Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika hali ambayo uhusiano wa karibu kati ya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea, Sonia Gandi amesema kuwa ukimya wa serikali ya India kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran, ni sawa na kuachana na “misingi ya maadili na mikakati” ambayo India imeijenga kwa muda mrefu.
Kiongozi huyo wa Chama cha Congress cha India, kupitia tahariri aliyoichapisha katika gazeti la The Hindu, ameyataja mashambulizi ya tarehe 13 Juni (sawa na 23 Khordad katika kalenda ya Kiirani) yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kuwa ni “haramu” na “uvunjaji wa mamlaka kamili ya Iran.”
Maoni yako